1Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:
2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.
3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.
4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.
5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.
6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”